Friday, February 24, 2017

Mama wa miaka 52 amtamani Mr Flavor


Lagos, Nigeria
MWANAMAMA mtata kwenye mitandao ya kijamii Kemi Olunloyo amewashangaza wengi baada ya kutumia akaunti yake ya twitter kumwomba penzi msanii nyota nchini Nigeria, Mr Flavor.

Olunloyo, 52, aliweka picha yake akiwa kwenye kivazi cha kimahaba na kusema kuwa angetamani kuwa pamoja kimapenzi na msanii huyo mwenye mvuto ambaye amekuwa akipendwa na wanawake wengi.

Hata hivyo Mr Flavor hakujibu maombi ya mwanamama huyo zaidi ya watu mbalimbali kuchangia mada hiyo wakiwa na hisia tofauti juu ya mwanamama huyo.

Wengine waliona kama huo ni ukosefu wa maadili huku wengine wakimsifu kwa kitendo chake cha kuweza kufunguka na kuepusha jaka la roho.


0 Comments: