Friday, February 24, 2017

Tiwa Savage kuja na kali ya mwaka


Abuja, Nigeria
MWANADADA mwenye ubora wake kwenye tasnia ya muziki nchini Nigeria, Tiwa Savage anaonekana kujiandaa kuachia ngoma yake mpya ambayo atashirikiana na baadhi ya wasanii wenzake wazawa.


Kupitia kwenye mtandao wake wa Instagram, Savage alituma picha akiwa na DJ Exclusive pamoja na Solid Star ambao kwa muonekano wa haraka walikuwa wakiandaa kitu kwaajili ya mashabiki zao.

Bado haijajulikana hasa ngoma hiyo itakuwa ni ya nani lakini wengi kwenye mitandao wanahisi kuwa itakuwa ni ya Savage ambaye tangu ajiunge na lebo ya Sony Music alikuwa bado hajatot wimbo wowote.

0 Comments: