Tuesday, February 14, 2017

Uwoya aandaa shindano la Kiss siku ya Valentine Day

STAA wa Bongo Move Irene Uwoya ameamua kuufanya usiku maalumu wa Siku ya Wapendanao yanii 'Valentine Day'leo na kuwa wa aina yake baada ya kuamua kuandaa mashindano ya kukisi kwa wapendao nao.

Uwoya anaweka wazi kuwa mshindi wa kukiss atapata nafasi ya kulala kwenye hoteli kubwa na kifahari kati kati ya Jiji la Dar es Salaam na kueleza kuwa anatarajia masupa staa kibao watahudhuria.
“Ni usiku wa wapendanao hata kama upo singo ni siku ya kuenjoy.Kutakuwa na mashindano ya kupiga kiss siku hiyo.Mwenyewe nitakiwa nahudumia VIP huku tukipata burudani murua kutoka kwa mwanadada Linah Sanga. Mapenzi ni bampa tu bampa,”anasema.
Kwa mujibu wa Uwoya ni kwamba kiingilio kwenye siku hiyo kitakuwa Sh 500,000 kwa watu muhimu na wengine Sh 20,000 kwa wale ambao ni wa kawaida.

0 Comments: