EBANA Irene Uwoya sio wa mchezo mchezo! Kisura huyu wa Bongo Movie katamka maneno ambayo wale vijana masharobaro hawatotaka kuyasikia hata kidogo.
Mchongo uko hivi, Irene aka Mama Krish alisema wanaume wenye sura mbaya ndio ambao wamekuwa wakiamsha hisia zake za kimapenzi zaidi kulinganisha na wale wanaoitwa mahandsome boy.
“Kitu ambacho hamkijui kuhusu mimi ni kuwa sijawahi kuvutiwa na wanaume wenye mwonekano mzuri, sielewi ni kwanini lakini wanaume wenye sura mbaya huwa wanaamsha hisia zangu za kimapenzi,”ameandika Uwoya.
Kisura huyo ameandaa shoo maalum ya Siku ya wapendanao ambapo ameahidi kueleza baadhi ya mambo ambayo watu hawayafahamu kuhusu yeye katika sekta ya mambo yetu yalee ya malavidavi.
0 Comments:
Post a Comment