ZARINA Hassan ‘ a.k.a Ze Bosslady amevunja ukimya kuhusu hatua ambayo wamefikia na baba wa watoto wake Nassib Abdul ‘Diamond’ katika suala la kufunga ndoa.
Mwanamama huyo wa Kiganda ameweka wazi kuwa kabla ya kufunga ndoa anataka kwanza yeye na Diamond kuboresha zaidi maisha yao kuliko yalivyo sasa huku akieleza kuwa Machi mwaka huu mpenzi wake atakwenda kujitambulisha rasmi kwa wazazi wake.
“Nataka ndoa yetu iwe ya gharama kubwa kwa Afrika Mashariki lakini kabla ya kufunga ndoa kuna mambo muhimu tunaweka sawa na mwenzangu.
“Pia Machi mwaka huu atakwenda nyumbani kwetu ili kujitambulisha rasmi wakati tunajiandaa na mambo mengine,”anasema.
0 Comments:
Post a Comment