Friday, February 24, 2017

Lawal asema baba yake anataka wajukuu



Lagos, Nigeria
MUIGIZAJI nyota wa kike nchini Nigeria, Moyo Lawal amefunguka na kusema kuwa yupo kwenye shinikizo la kuingia kwenye ndoa kutoka kwa familia yake.

Akifanyiwa mahojiano na kipindi cha Green Views, Lawal alisema kuwa baba yake amekuwa akimwambia kuwa anataka kuona wajukuu hivyo ni wajibu kwake afanye upesi kuolewa.

"Nimekuwa nikishinikizwa kuingia kwenye ndoa na kwasababu hiyo ni lazima nimpe furaha baba yangu kwakuwa mimi ndiyo mtoto mkubwa kwenye familia,"anasema.

Anasisitiza kuwa hatokuwa na haraka kubwa hadi pale atakapopata mtu sahihi wa kuingia nae katika ulimwengu huo.

0 Comments: