Friday, February 24, 2017

'Sina mpango na masharobaro, najituliza kwa Sugar Dady'

PRETORIA, Afrika Kusini
KING'ASTI wa nguvu kutoka ardhi ya Madiba, Blue Mbombo ni kama ameamua kuwafungia vioo vijana ambao wamekuwa wakimaliza 'sound' zao kumrushia ndoano baada ya kusema kwa sasa hana mpango na masharobaro hao.

Ubuyu wetu unasema kuwa Blue ambaye alikuwa nje ya mahusiano ya kimapenzi tangu aachane na Rapa K2 sasa ameamua kurejea kwenye ulingo wa mahaba lakini safari hii ikiwa kivingine kwanin ameamua kutoka na mwanaume mwenye umri mkubwa.

"Nimekua kwenye mahusiano na vijana nimegundua wengi wao hawapo serious na mapenzi, sasa nipo na mwanaume mtu mzima wapo watakaosema nahitaji fedha kutoka kwake, la hasha!

"Mimi ni mwanamke mfanyabiashara sitaki pesa kwa wanaume zaidi nahitaji anifundishe namna ya kuongeza pesa,"anasema Blue.

0 Comments: