Friday, February 24, 2017

Angelina Jolie anakula hadi Mende?

NEW ORLEANS, Marekani
NAJUA kwamba unafahamu Angelina Jolie ni mama ambaye amejaliwa  vipaji lukuki huku akiwa miongoni mwa waigizaji wa kike wanaopokea mtonyo mkubwa Hollywood.
Sasa nakupenyezea kitu kingine ambacho hukijui kuhusu kimwana huyu ambaye kila kukicha amekuwa akionekana bado kig'ori, ipo hivi pamoja na urembo wake unaambiwa Angie haogopi kula nyama ya wadudu wanaotisha, ambapo katikati ya wiki hii alinaswa akila nyama ya nyoka na mende katika mgahawa fulani hivi.

"Kwangu mimi hizi ni vitoweo ambavyo vimekuwa vikiuburudisha moyo wangu, kwangu mimi kutafuna mende, ng'e na nyota ni sehemu yangu ya kupata mlo utakaoulinda mwili wangu usinenepe hovyo,"anasema Angelina.

0 Comments: