Friday, February 24, 2017

Kareena atamba kutwaa tuzo



NEW DELHI, India
SUPASTAA wa  Boolywood, Kareena Kapoor amesema ana imani kwamba filamu yake ya Rangoon itatwaa tuzo ya filamu bora ya mwaka na hivyo anajiandaa kukabidhiwa tuzo yake.

Kareena ambaye amempa shavu mumewe Saif Ali Khan katika filamu hiyo aliamua kufunguka ya moyoni katikati ya wiki hii kuhusu ubora wa kazi yake hiyo huku akisema atashangaa endapo hatotwaa tuzo yoyote na filamu hiyo.

"Nimefanya kazi nyingi sana Vishal ni muongozaji bora kabisa ndani ya Boolywood lakini uwepo wa Saif umeongeza ubora mkubwa.

"Nani ambaye hajui namna ambavyo mtu huyu hukamua kwenye filamu anazocheza? Ni zamu yangu, ni zamu ya Rangoon mwaka huu,"anasema Kareena.

0 Comments: