Tuesday, February 14, 2017

Darassa atokwa povu video za Bongo kufanana


‘HITMAKER’ wa kichupa cha muziki, Darassa amefunguka kuwa hakuna kitu kinachomboa kwenye muziki hivi sasa kama kuendelea kuigana na kufanana kwa baadhi ya vitu kwenye video nyingi za kibongo.

Darassa alitokwa na povu hilo katikati ya wiki hii ambapo alisema video nyingi zimekuwa zikionesha mandhari zinazofanana, kutumia magari ya aina moja sambamba na warembo wanaouza sura kwenye vichupa hivyo.
“Inanipa taabu kuona mtu ambaye katokea kwenye video yako ndiyo huyo huyo kwenye video ya msanii mwingine, hii inafanya kupoteza mvuto kwa video zetu kwa mashabiki ambao wamekuwa wakihitaji kushuhudia ubunifu kutoka kwetu,”anasema Darassa.


0 Comments: