
HITMAKER wa ngoma ya Kokoro, Rich Mavoko amesema ushirikiano, upendo na kusaidiana ndio staili ya maisha ndani ya familia ya Wasafi inayoongozwa na Supastaa Diamond Platnumz.
Mavoko anasema maisha ndani ya kundi hilo lililoteka muziki wa Bongo Fleva ni mazuri licha ya kwamba wao kama binadamu lazima wagongane kimawazo lakini ikiwa ni migongano yenye kujenga na siyo kubomoa.
Anasema tangu ajiunge na lebo hiyo muziki wake umepiga hatua kubwa sana kutokana na kuchezwa chaneli za nje.
“Kiukweli maisha ndani ya WCB, huwezi kusema hatugombani lakini si kila siku na mara nyingi ni katika kujenga muziki wetu zaidi, zaidi ni lebo ambayo kupata mafanikio ni rahisi kutokana na watu waliotuzunguka (Tale na Salaam) kuelewa biashara ya muziki kwa upana,”anasema staa huyo wa Marry me.
0 Comments:
Post a Comment