Friday, February 17, 2017

Mwana FA aingilia ugomvi wa Nash Mc, Profesa Jay

KIMENUKA! Kama ilivyo ada ya muziki wa Hip Hop kumchana mwenzako ni jambo linaloruhusiwa sasa wiki hii michano ilikuwa kati ya Mkali wa Rap, Nash Emcee na Mbunge wa Mikumi, Profesa Jay kabla ya Mwana FA kuingilia kati.

Stori ipo hivi, Nash alimuuliza Profesa hivi Singeli imeshakwenda kimataifa? Hiyo ni basi Jay akajibu hivi, “Nash aliuliza singeli imekwenda kimataifa? Nilitegemea angeuliza kwanini Hip Hop haivuki boda? Badala ya kujiuliza tumekosea wapi tunakua wavivu kufikiri, achene wivu wa kijing,”
Nash akajibu tena akamwambia Profesa “Nina uhuru wa kuongea nachotaka muhimu nisivunje sheria, hakuna yeyote wa kunipangia cha kuuliza sina nidhamu ya woga,”
Basi baada ya mapovu hayo ndipo FA akaingilia na kuandika, “Chemsha Bongo, Nuikusaidiaje, Jina langu, Ndio mzee, Zali la Mentali , Hapo vipi na nyingine nyingi come on tusimkosee hesshima na adabu huyu mzee,” Akilenga kumkosoa Nash kwa kubishana na Profesa.


0 Comments: