
KIMWANA aliyejipatia umaarufu na kipindi chake cha Ala za Roho kinachorushwa na Clouds Radio, Diva ametoa kali ya mwaka baada ya kusema eti hawezi kutoka kimapenzi na mwanaume asiyejua Kiingereza.
Diva anasema huvutiwa zaidi na mwanaume anaetema yai la kizungu kwa sababu huonekana kuwa ni wenye maendeleo na waliopiga hatua zaidi kuliko wanaozungumza Kiswahili muda wote.
Anasema kipindi chake hicho ambacho ni cha mapenzi ndicho humkutanisha na wanaume wake wengi.
“Aisee sipendi mwanaume ambaye hajui kuongea Kiingereza, wanakuwa wapo makini, mimi muda mwingi nazungumza Kingereza kama yeye atakua hajui itakuwa shughuli kati yetu na ndio maana sina muda nao wasiojua kizungu,”anasema Diva.
Mrembo huyo kwa sasa anajibebisha na penzi la mkali wa sauti, Heri Muziki na hiyo ni baada ya kumpiga chini mtu mzima GK.
0 Comments:
Post a Comment