Friday, February 24, 2017

Jennifer Lopez asema Drake ni mdogo kwake

Washington, Marekani

MKONGWE wa muziki nchini Marekani, Jennifer Lopez amefunguka kwa mara ya kwanza kuhusu mahusiano yake na rapa Drake.

Akizungumza katika kipindi cha runinga cha Ellen, muimbaji huyo amekanusha kuwa na mahusiano na Drake kwa kusema kuwa hawezi kuwa na mahusiano na vijana.

"Mimi siwezi kuwa na mahusiano na vijana wadogo, napenda kujichanganya na watu na kutoka nao kwaajili ya matembezi lakini hakuna cha ziada baada ya hapo,"anasema.

Wakati huo huo Jennifer aliulizwa kama alikuwa pamoja na rapa huyo siku ya Wapenda Nao ambapo alisema kuwa hawakuwa pamoja kwakuwa msanii huyo yupo kwenye ziara kwasasa.

0 Comments: