Friday, February 24, 2017

Drake akana kumtusi Minaj

California, Marekani
NYOTA wa rapa nchini Marekani, Drake ameonekana kuanza kujisafisha kwa msanii mwenzie Nicki Minaj baada ya kutokuwa na mawasiliano naye kwa takribani miaka miwili.

Akizungumza katika mahojiano na kituo cha redio ya OVOSOUND, rapa huyo alisema hawezi kumvunjia heshima Nicki kwa njia yoyote ile na kukanusha kuwa aliwahi kumuita kwa majina mabaya.

"Siwezi kumtusi Mick kwa kuwa ni mmoja kati ya watu ambao nina waheshimu zaidi,"anasema.
Rapa huyo aliwahi kutuhumiwa kumtusi Minaj wakati akiwa kwenye mahusiano na Meek Mill kwenye moja ya nyimbo zake za diss kwa rapa huyo wa Philladelphia.

0 Comments: