Friday, February 17, 2017

Hee! kumbe Amber Rose, Wiz Khalifa bado hakijaeleweka

California, Marekani
DIVA wa muziki nchini Marekani, Amber Rose amekanusha taarfia za kuwa amerudiana na mumewe mwanamuziki Wiz Khalifa.
Tetesi za wawili hao kurudiani zilianza kuzagaa kwenye mitandao ya kijamii tangu wiki iliyopita baada ya picha za wawili hao kuzagaa wakiwa wamepena busu la mahaba mdomoni.

Tukio hilo la kupeana busu hilo lilinaswa kwenye ukumbi wa siku ya sherehe za ugawaji wa tuzo za Grammy. Baada ya picha hizo kuzagaa watu walijiongeza na kusema kuwa tayari kimeeleweka.
Hata hivyo mwenyewe Amber Rose ameibuka na kueleza yeye ni mwanamuziki kama ilivyo kwa Wiz Khalifa hivyo wao bado ni familia moja katika masuala ya kazi na si vinginevyo.


0 Comments: