
KWA Dyana Nyange ni tofauti! Hii ndio unayoweza kuileza kwa mwanadada huyo ambaye yupo tofauti na mastaa wengine wenye tabia ya kuweka picha na habari za watoto wao mitandaoni.
Dayna Nyange ambaye jina lake halisi ni Mwanaisha Said anasema kuwa haoni sababu ya kila jambo linalomhusu yeye au familia yake aliweke hadharani na hasa kwenye mitandao ya kijamii.
“Ninaye mtoto mwenye umri wa miaka 10 lakini sijawahi kumuweka kwenye mitandao ya kijamii kila siku kama ambavyo wengine wanafanya.
“Na si kwenye mitandao tu hata kwenye vyombo vya habari sijawahi kumuweka maana hakuna ulazima wa kufanya hivyo,”anasema.
Anafafanua zaidi amefungua akaunti ya Instagram mtoto wake lakini hiyo ni kwa ajili ya mambo binafsi na hasa kwa ajili ya kuweka picha zake kama kumbukumbu.
0 Comments:
Post a Comment