Tuesday, February 14, 2017

Chemical atamani kuifanyia remix Muziki wa Darassa


RAPA wa kike, Chemical anaetamba na ngoma yake ya Mary Mary ameamua kuweka hadharani traki zake kali ambazo anatamani leo kesho apate shavu la kuzifanyia remix.

Chemical amezitaja ngoma hizo kuwa ni Muziki ya Darassa aliompa shavu mkali wa R&B, Ben Pol na ule wa Sisikii alioimba Maua Sama huku akisema anaamini akizifanyia remix zitatoboa ile mbaya.
“Kuna wasanii wanajua kutoa ngoma kali ambazo zinaweza kukufanya utamani kuzifanyia remix, kuhusu kushindanishwa na rapa wengine sipendi na naamini baada ya muda uwezo wangu utajidhihirisha zaidi,” anasema Chemical.




0 Comments: