Tuesday, February 14, 2017

Mziwanda aweka hadharani majina atakayompa mwanae


WASWAHILI wanaita kihoro cha Mtoto, Sikia mkali wa mastori mitandaoni, Nuh Mziwanda amefichua kuwa tayari anayo majina ya mtoto wake ambaye anatarajia kumpata hivi karibuni kama Mungu akijalia mkewe kujifungua salama.

Mshawasha huo ndio ambao umemfanya Nuh kukimbilia kwenye Instagram yake na kuandika kuwa endapo mtoto huyo atakua wa kiume basi atapewa jina la Travis na kama ni wa kike atampa jina la Malikah ambalo pia ni la mtoto wa Mwana FA.



0 Comments: