SUPA-STAA Wema Sepetu a.k.a Madam amesema anachukizwa na tabia ya baadhi ya watu ambao wamekuwa wakimtolea lugha za kejeli na matusi mwigizaji Anti Azekiel.
Kupitia mtandao wake wa kijamii wa instagram Wema ametumia nafasi hiyo kueleza wazi anachukizwa na hao wenye tabia ya kumshambulia Anti Ezekiel.
Taarifa ni kwamba baada ya Anti Ezekiel kuhudhuria sherehe ya kuzaliwa ya mzazi mwenza wa Nasib Abdul ‘Diamond’ Zarinah Hassan kumekuwa na maneno mengi yakielekezwa kwa Anti.Hivyo Wema anasema wanaomtusi Anti Ezekiel ni vema wakaacha kwani binafsi wanamchukiza sana.
0 Comments:
Post a Comment