Chicago, Marekani
MASTAA wa muziki nchini Tiny na T.I inadaiwa kuwa wanaweza wasiachane hata baada ya mwanamke kuomba talaka.
Ripoti mpya imedai kuwa wawili hao wamekuwa kwenye maelewano mazuri tangu Tiny adai talaka yake, Dec. 7, mwaka huu na wamekuwa pamoja kwa ukaribu zaidi.
Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali vya habari wawili hao walisherehekea Sikukuu ya Krismasi pamoja na familia yao.
Wamekuwa pamoja kwa miaka 20 lakini walifunga ndoa rasmi mwaka 2010 na hadi sasa wana watoto watatu pamoja ambao ni King, Major, na Heiress Harris.
Hata hivyo T.I. alikuwa na watoto wengine wa nje ya ndoa ambao ni Messiah, Domani, na Deyjah Harris na Tiny ana binti aliyemzaa kwenye uhusiano uliopita, Zonnique Pullins.






0 Comments:
Post a Comment