Friday, January 27, 2017

Snura atamani kipimo cha DNA ...

MSANII Snura Mushi ambaye ni mama wa watoto wawili ameiomba Serikali kuangalia uwezekano wa kupunguza gharama za kipimo cha vinasaba (DNA) ili watu wa hali ya chini waweze kumudu.
Snura ametoa ombi hilo hivi karibuni ambapo anafafanua kuwa anatamani kuona gharama za kipimo hicho zinakuwa nafuu ambazo wengi wenye kukihitaji kukipata na hasa kwa watu wa kipato cha chini wanashindwa kwasababu ya bei.

Anasema kumekuwa na tabia ya baadhi ya wanaume kukataa mimba , hivyo njia pekee ni kipimo cha DNA ambacho kinaweza kutoa jibu sahihi lakini inakuwa ngumu kukitumia kipimo hicho kwasababu ya gharama.
“Ni vema Serikali ikaangalia namna ya kupunguza gharama za kipimo cha DNA ili kutoa fursa kwa wengi kukitumia na kupata ufumbuzi wa hii changamoto ya watu kukataa mimba,”anasema.

0 Comments: