Friday, January 27, 2017

Mke wa Mziwanda amtolea uvivu Shilole


MKE wa msanii wa muziki wa kizazi kipya Nuh Mziwanda, Nawal ameamua kujibu mapigo dhidi ya Shilole na kumweleza anachokiona ni kama vile atapatapa tu na hana ubavu wowote kwake.

Shilole aliwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Nuh Mziwanda lakini waliachana na hapo ndipo msanii huyo anayetamba ni kibao cha Jike Shupa alipoangukia kwenye penzi la Nawal ambaye ndio mkewe wa ndoa kwa sasa.
Nawal ambaye naye si wa mchezo mchezo ameamua kueleza kuwa anamwamini sana Nuh Mziwanda na anachokiona kwa Shilole ni kama vile anahangaika tu huku akieleza kuwa yeye ni baab kubwa zaidi yake. “Hanitishi na hanifikii na ninachokiona anatapatapa tu”anasema Nawal wakati anapiga stori kwenye kipindi cha Shilawadu.


0 Comments: