Friday, January 27, 2017

Rayvanny wa WCB apanga kuachia ngoma mpya


KIRAKA anayetamba na lebo ya WCB, Rayvanny amesema baada ya kutoka na kufanya vizuri na ngoma ya Kijuso aliyopewa shavu na memba mwenzake, Queen Darleen nae amejipanga kuachia rekodi yake.

‘Hitmaker’ huyo wa ngoma ya Kwetu na Kiki amefichua kuwa ana ngoma nyingi ambazo anaamini akiziachia zitafanya vizuri lakini kwa sasa anasubiri baraka kutoka kwa uongozi wake ili kuachia rasmi.
“Mashabiki wangu soon nitaachia ngoma yangu mpya ambayo nawaahidi kuwa itakua si mchezo lakini kwa sasa kuweni na subira kwanza itoke video ya Kijuso kisha baada ya hapo kijana wenu nitawabariki na chuma kikali,” Anasema Rayvanny.


0 Comments: