Friday, January 27, 2017

Ray C ajipanga kivingine , aacha ‘unga’


AMEAMUA! Kama ulikuwa hujui kitu kuhusu maendeleo ya afya ya Ray C au unadhani bado anabwia unga basi unajidanganya, kimwana amependeza na ule mwonekano wake mzuri umerejea.
Stori ipo hivi, katikati ya wiki hii, Ray C a.k.a Kiuno bila mfupa, alitupia picha zake kwenye akaunti yake ya Instagram zikimuonesha jinsi anavyoonekana hivi sasa ambapo amedhamiria kurudi kamili kwenye muziki ambapo anarekodi ngoma zake kwenye studio za Wanene Entertainment.

“Nimeanza kumpenda tena huyu dada Ray C jamani sitaki kumdhuru tena na yale mavitu hata kwa sumu na bunduki siwezi kurudia, nataka azidi kunivutia zaidi kila nimuonapo kwenye kioo,”anaandik Ray C.


0 Comments: