
MBWANA Mohamed a.k.a Mb Dog ni moja kati ya wasanii ambao walifanikiwa kutikisa kwenye anga la muziki wa Bongo Fleva.
Ni msanii ambaye amepita kwenye changamoto lukuki kwenye tasnia hiyo na sasa amezizoea na haoni kama kikwazo cha yeye kurejea kwenye ushindani katika muziki huo.
Akizungumza hivi karibuni, msanii huyo anasema kwa sasa anajiandaa kuachia ngoma mpya ambayo anaamini itafanya vema na kuhimili ushindani uliopo.
“Kwa sasa nasubiri katika kampuni yangu msanii mmoja aachie ngoma yake na kisha nami niachie yangu ambayo tayari imekamilika kwa asilimia 100,”anasema.
Anasema kwa namna anavyoona soka la muziki limekuwa zuri kwani wasanii wengi kujituma na kufanya kazi nzuri ili kufanikisha ndoto zao kimuziki.
Anaongeza bado anao uwezo wa kufanya vizuri katika game kwani hakuna jipya bali ni kuongeza ubunifu na kuangalia mahitaji ya mashabiki.
0 Comments:
Post a Comment