
Magendela Hamisi
JUDITH Wambura maarufu kwa jina la Lady Jay Dee ni miongoni mwa wasanii wa kike ambao wamefanikiwa kimaisha
Sifa kubwa ya mwanadada huyo hajawahi kuchuja kwenye muziki wa kizazi kipya.Kila kukicha anakuwa mpya na hiyo imemfanya endelee kubaki kwenye chati za juu.
Wakati wakongwe wengine wamepotea kwenye muziki yeye anaendelea kung’ara.Hajakosea kujiita Komandoo.
Siku za karubuni amazungumza na safu hii ambapo ameleeza mambo mengi kuhusu muziki wake.Amekuwa kwenye muziki kwa zaidi ya miaka 16.Hivyo ana mengi ya kuzungumza.
Swali: Wengi wamekusaidia na wengine leo hauko nao,hali ikoje?
Jibu: Kila mmoja niliyekuwa naye katika maisha yangu alikuwa na mchango wake.Hivyo ninapoachana nao huwa najipanga upya na kufanya vema katika kazi zangu za muziki na ndio maana nafanikiwa licha ya kupita katika changamoto lukuki.
Swali: Njia gani unafanya kubaki na mashabiki wako?
Jibu: Kwanza naheshimu kazi yangu na kila ninachokifanya na watu uwaoneshe kuwa unaeshimu unachokifanya na kufanya kazi nzuri, mara kadhaa nakaa muda mrefu bila kuachia wimbo na baadhi ya wadau wanasema pengine nimefulia.
Huwa sifanyi kazi kwa kulipua, bali nakaa na kuumiza kichwa nini nifanye ili kuendelea kutoa kazi nzuri.Mashabiki wangu ni sehemu ya watu muhimu kwangu na ninawaheshimu siku zote.Kabla ya kutoa nyimbo yangu huwa nafanya tafiti na hiyo imenisaidia kutoa kazi zenye ubora.
Swali: Kuna mtu anakuandikia mashairi ili uendelee kubaki kwenye chati?
Jibu: Nafanya kazi na watu wengi na katika hilo siwezi kukataa kuwa hakuna watu wanaoniandikia, lakini kwa asilimia 95 ya nyimbo zangu huwa naandika mwenyewe na zaidi kutokana na mambo yanayozunguka hasa maisha yangu binafsi.
Pia inafika wakati sina hisia za kuandika hapo ndipo nakaribisha mawazo ya watu wengine ambao nasaidiana nao katika kuandika ili kutoa kitu kizuri kitakachoshika mashabiki.
Swali:Je, una mpango wa kusaidia wasanii wengine?
Jibu: Sina plani ya kusimamia wasanii kwa sababu kila mmoja anapoamua kufanya hivyo anakuwa na muda wa kufanya na kujipanga vema katika mchakato huo, sijui siku za mbele.
Swali: Bendi yako bado ipo?
Jibu:Bendi ipo na ndio nazunguka nayo katika maonesho mbalimbali, hivyo hakuna tatizo kwenye hilo.
Swali: Unaendelea na ratiba ya shoo za kila wiki?
Jibu:Sifikirii kuendelea kufanya shoo kila wiki labda kwa mwezi mara moja kwani biashara inabadilika na nimefanya hivyo kwa muda wa miaka saba biashara haiwezi kwenda hivyo kila siku.Upepo ukibadilika nami nabadilika ili nifikie mafanikio.
Swali: Upo kwa muda mrefu,kuna msanii yoyote amewahi kukuhitaji?
Jibu: Kwa namna ambavyo nimejiweka na wengi wanvyoniona wananiheshimu na hawawezi kuningia kirahisi,wananiheshimu sana na wananiona kama dada wa taifa ingawaje huwezi kukosa changamoto hiyo.
Swali:Umewahi kufanya kazi na Ali Kiba, vipi kwa Diamond?
Jibu:Sina tatizo na mtu yeyote anayetaka kufanya kazi na mimi na milango iko wazi kwa msanii yoyote yule.
Swali: Je, umeshawahi kufanya naye kazi?
Jibu: Nachoweza kusema tu nipo tayari kufanya naye kazi na akinihitaji sina tatizo.
kupitia muziki wa kizazi kipya.
0 Comments:
Post a Comment