Wednesday, January 25, 2017

Jide atoa somo kwa wanaoteswa na mapenzi

DADA mkuu wa Bongo Fleva, Judith Wambura a.k.a Jide amesema wanawake wengi wamekuwa waoga kuingia kwenye mahusiano mapya ya kimapenzi  pindi wanapoachana na wenza wao wa mwanzo.

Jide anasema wasichana wengi wamekuwa wakishindwa kuanzisha mahusiano mapya kutokana na woga na kutojiamini jambo ambalo limekuwa likiwaumiza wengi wao.
“Kama unakuwa upo kwenye mahusiano ambayo huoni faida yake huku ukiteseka na kuumia ya nini kung’ang’ania? Hayo mambo ya kwamba mmejenga pamoja isiwe sababu ya kuumia,”anasema Jide.


0 Comments: