HUWEZI kuamini! Eti kumbe Meneja wa WCB, Sallam SK licha ya utofauti uliopo baina ya lebo yake na Ali Kiba lakini jamaa unaambiwa anaukubali wimbo wa Mac Muga kinoma.
Sallam ambaye alitumia muda wake kuchat na kujibu maswali ya mashabiki wake kupitia akaunti yake ya IG, ambapo walipomuuliza wimbo gani wa Kiba anaukubali alijibu ‘Mac Muga’ .
“ Nyimbo zote za WCB nazikubali mwanangu, ile ndio biashara yangu hivyo lazima nizikubali, kuhusu msanii wa nje ya lebo yetu naemuelewa ni Ben Pol na ngoma yeke ya Moyo Machine naukubali kinoma,” amesema Sallam.
Sallam pia anasema anamkubali Barnaba huku ngoma yake anayoikubali ni Lover Boy huku akifichua kuwa Harmonize yupo njiani kutoka na rekodi mpya.
0 Comments:
Post a Comment