Sunday, January 1, 2017

‘Bwana mpya’ amponza Shilole Instagram


STAA wa muziki wa kizazi kipya amejikuta akishambuliwa na mashabiki wake wa muziki baada kuandika utani kwenye mtandao wake wa kijamii kuwa anachojivunia mwaka 2016 ni kupata mpenzi mpya.Mashabiki wa muziki nchini baada ya kuona kilichoandikwa na Shilole wakaamua kumtolea uvivu kwa kumpa makavu na kumwambia hawakufurahishwa na alichoandika mtandaoni.Shilole kwenye mtandao wake wa Instagram hakusita kueleza anachojivunia mwaka 2016 ni kupata bwana mpya.Hata hivyo Shilole amekaa kimya kwani hakutaka kuwajibu mashabiki wa muziki wake.


0 Comments: