Sunday, January 1, 2017

Dimpoz azungumzia kuondoka kwa Mubenga

NYOTA mwenye dimpoz za kutosha, Omary Nyemo a.k.a Ommy Dimpoz amesema kuondoka kwa aliyekuwa meneja wake, Mubenga hakujaathiri chchote ndani ya kampuni yake ya PKP.
Stori ipo hivi, Dimpoz anasema licha ya yeye na Mubenga wametoka mbali tangu wimbo wake wa kwanza wa Nai nai lakini sasa kila mtu anafanya kazi kivyake baada ya meneja huyo kuondoka kwa hiyari yake mwenyewe.

Anasema hakuna ugomvi baina yao na kilichotokea na hali ya kawaida kwa mtu yoyote kwani hata majumbani watoto wakikua huondoka na kwenda kujitegemea hivyo anamtakia maisha mema Mubenga kwani wameishi vizuri.
“Sasa hivi naangaika kufanya muziki ambao utakuna mashabiki wangu kama ulivyoona nimetoa Kajiandae nikiwa na Kiba na imefanikiwa bila uwepo wa Mubenga hivyo hakuna pengo lolote la yeye kuondoka,”anasema Dimpoz.

0 Comments: