Sunday, January 1, 2017

Aunty Ezekiel hataki tena kubusu kwenye filamu


MKALI wa filamu za kibongo a.k.a ‘Bongo Muvi’ Aunty Ezekiel, ametoa msimamo wake kuwa kwa sasa hataweza tena kuigiza sehemu inayohitaji Kubusu maana sasa maisha yake ni tofauti na yale ya awali.

Aunty Ezekiel kwa sasa ametoa filamu mpya inayokwenda kwa jina la Chritmass Eve, anasema sababu za kufikia uamuzi huo ni majukumu aliyonayo ya kuelea familia na malezi kwa mtoto wake.
“Nimechenji baada ya kuzaa, nimekuwa na mawazo tofauti, nimerudi nyuma mara mbili hata ikitokea kwenye movie natakiwa ku-kiss, najifikiria sana hivi mwanangu akiona atafikiria nini,”anasema.
Aunty Ezekiel ambaye alikuwa anahojiwa na kituo cha runinga cha EATV Aunty anasisitiza anapokuwa kwenye muvi kabla ya kukisi anaanza kufikiria mtoto wake na kutoa mfano kuwa hawezi kuigiza kama ambavyo amefanya kwenye filamu ya House girl.
“Nimeshakuwa mtu mzima ,hivyo kuna mambo mengi ambayo nimefanya siku za nyuma siwezi kufanya tena  kwani nimeacha.Siwezi kuishi maisha ya kitoto wala kuishi kwa skendo kwani hakuna faida,”anasema.


0 Comments: