Sunday, January 1, 2017

Yvonne ataja rangi ya nguo aipendayo


KING’ASTI ambaye kama asipoongelewa mitandaoni basi haoni raha,
Katikati ya wiki hii mrembo huyo alipiga picha akiwa amevalia gauni lililomshika mwilini na kutupia katika mtandao wake wa Instagram na kuwataka mashabiki wake kumpa maksi kama amependeza au hajatokelezea.

Basi ndani ya dakika kadhaa picha hiyo ilikuwa imetimiza ‘likes’ 40,000 huku mashabiki wake wakimsifia kuwa pamoja na umri kumsonga mbele bado ameendelea kuwashika na urembo wake.
Yvonne alitumia mtandao huo kuwatakia mashabiki wake heri ya Krisimasi na mwaka mpya na kuwaambia kuwa wamekuwa katika kichwa chake kwa miaka yote kutokana na sapoti kubwa ambayo wamekuwa wakimpatia katika kazi zake.


Yvonne Nelson msimu huu wa sikukuu amekuja kivingine baada ya kusema kuwa kama kuna mtu anataka kumletea zawadi ya nguo basi iwe ya rangi nyeusi.

0 Comments: