Saturday, February 14, 2015

John Kitime awasafishia njia Mashujaa

BENDI ya muziki wa dansi ya Mashujaa Musica ‘Wanakibega’ kwa sasa ipo kamili baada ya kupigwa msasa wa wiki mbili na nguli wa muziki huo nchini, John Kitime.
Uongozi wa Mashujaa ulifikia uamuzi wa kutafuta mkufunzi ili kuifanya bendi hiyo kuwa katika kiwango cha juu.
Meneja wa bendi hiyo, Martin Sospeter, alisema bendi hiyo kwa sasa imekamilika kila idara na ina mabadiliko makubwa, tofauti na ilivyokuwa awali, kwa sasa ni bora zaidi.

0 Comments: