MWIMBAJI
wa muziki wa mduara nchini, Ally Ramadhani ‘AT’, amejivunia kutoa wimbo
wa kwanza kwa mwaka huu na kukubaliwa kwa kiasi kikubwa na mashabiki
wake, hivyo kumuonyesha njia ya mafanikio.
AT alisema kuwa kitendo hicho kimemfurahisha sana na kuuona kama mwaka huu utakuwa ni wa mafanikio makubwa kwake, kwani siku chache baada ya kuuachia wimbo wake huo wa Sijaona umekuwa ukipigwa kwa kasi sana kwenye studio mbalimbali za redio.
“Huu ni mwanzo mzuri kwangu, nina imani nitafanya vizuri zaidi ndani ya mwaka huu, kwani licha ya kukubalika huku Tanzania Bara pekee, hata Zanzibar umekuwa ukifanya vizuri, najivunia kwa hilo,” alisema.
Alisema mipango yake mikubwa kwenye muziki wake huo kwa sasa ni kufikia malengo aliyojiwekea kwa mwaka mzima, ili atimize ndoto zake za kuwa msanii wa kimataifa na kipato kikubwa.

0 Comments:
Post a Comment