Saturday, February 14, 2015

Ali Kiba mbioni kuachia albamu

WAKATI baadhi ya wasanii wakikimbia kutoa albamu kutokana na madai kwamba hazina faida, msanii wa muziki wa bongo fleva nchini, Ally Kiba, amesema yupo mbioni kuachia albamu yake mpya ambayo bado hajaipa jina.
Alisema, yupo katika hatua za mwisho kukamilisha albamu hiyo ambayo ataitambulisha kabla ya kuachia nyimbo zake nyingine katika vituo mbalimbali vya redio na runinga.
“Nitakapo itambulisha rasmi ntakuwa tayari nimeshapata jina na nitawataja wasanii niliowashirikisha wa ndani na wale wa kimataifa,” alisema.
Alisema, baada ya kumaliza shoo yake kwenye Tamasha la Sauti za Busara ndipo ataanza harakati za kuitambulisha albamu hiyo, ikiwemo mikoani na nchi mbalimbali kadri itakavyowezekana.

0 Comments: