Saturday, February 14, 2015

Queen Suzy kuacha kucheza shoo

MCHEZA Shoo wa bendi ya FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’, Suzan Chubwa ‘Queen Suzy’, amesema yupo mbioni kuachana na kazi hiyo ili ajikite katika uimbaji binafsi.
Dansa huyo wa muda mrefu alisema kuwa kwa sasa anaweka mambo yake sawa na yatakapokamilika ndipo ataanza rasmi kuimba nyimbo zake.
“Nataka kufanya kazi zangu binafsi, kwani nimechoka kuajiriwa, nitakuwa naimba nyimbo zangu ya miondoko kama ya Fally Ipupa na ragger dance,” alisema.
Alisema, anaamini kipaji chake cha kuimba, licha ya kujikita katika unenguaji, huku akiwataka mashabiki wake kumtia hamasa ili afanye vema katika kazi yake mpya ya kuimba.

0 Comments: