Friday, October 17, 2014

Zoe Saldana kuzaa watoto mapacha

LOS ANGELES, Marekani
MWIGIZAJI nyota wa filamu ya Avatar, Zoe Saldana, amethibitisha kuwa atajifungua watoto wawili mapacha katika ujauzito wake na mumewe, Marco Perego.
Staa huyo mwenye umri wa miaka 36, awali alithibitisha furaha yake ya kupata watoto hao wakati wa mahojiano na jarida la E! News mwezi huu. 

Hata hivyo, mwimbaji Britney Spears amempongeza mke huyo wa Perego alipoulizwa na jarida la Entertainment Tonight kama atacheza filamu nyingine na Saldana ambapo Spears alisema: "Nani anajua, hilo ni wazo zuri sana, lakini yeye ni mjamzito wa mapacha nina hakika atapiga hatua kubwa baadaye.
“Saldana ana msisimko mkubwa kuzaa watoto wawili na daima anataka familia kubwa,” chanzo kingine kiliiambia Us Weekly.

0 Comments: