Friday, October 17, 2014

Iggy Azalea kuwania tuzo ya mvuto


LOS ANGELES, Marekani
RAPA kutoka Australia, Iggy Azalea ameteuliwa kuwania tuzo sita za American Music, ikiwemo tuzo ya msanii mwenye mvuto kwa mwaka huu.
Azalea ambaye ameingia kwenye bifu na mwimbaji mkongwe, Snoop Dogg, atawania tuzo ya msanii bora wa mwaka na Perry, Pharrell Williams, Lorde, Legend na Beyonce.
Aidha, waimbaji kama John Legend, Pharrell Williams na Katy Perry hawakuachwa mbali katika tuzo hizo ambapo watawania tuzo tano kila mmoja, wakifuatiwa na mwimbaji kutoka taifa la New Zealand, Lorde anayewania tuzo nne.
Staa Charli XCX na mwimbaji Jason Derulo, walitangazwa kuwania tuzo hizo katika makundi matano, huku Charli akitumbuiza katika hafla hiyo kwa mara yake ya kwanza.
American Music Award itafanyika Novemba 23 huko mjini Los Angeles.

0 Comments: