Friday, October 17, 2014

Davido kushindana na Usher, Chris Brown na Beyonce

LAGOS, Nigeria
STAA wa Nollywood, Davido ametangazwa kuwa mmoja wa wasanii kutoka Afrika watakaowania tuzo za Soul Train, zitakazofanyika mwezi ujao.
Staa huyo wa Nigeria atashindania tuzo ya msanii bora wa kimataifa (Best International Performance) iliyoingiza kibao chake cha 'Aye', na waimbaji kama Machel Montano, Nico & Vinz, Sam Smith, Shaggy na Ziggy Marley. 

Soul Train Awards zitatolewa siku ya Jumapili ya mwezi, Novemba 30 ambapo vipengele vingine vitakavyowaniwa ni pamoja na albamu bora, wimbo bora, msanii bora wa kike /kiume, video bora, mwandishi bora wa wimbo, wimbo bora wa Hip-hop, wimbo wa kushirikiana na nyingine nyingi.

0 Comments: