Friday, October 17, 2014

Kauli ya Chris Brown yakera wengi


MIAMI, Marekani
STAA Chris Brown ametuma ujumbe uliowakera mashabiki wake kwenye mtandao wake wa Twitter, kuhusiana na ugonjwa wa Ebola.
Chris aliandika kuwa; “Sijui, lakini nadhani janga la Ebola ni njia mojawapo ya kudhibiti idadi ya watu duniani, janga hili linatisha kweli.”
Ingawa baadaye aliandika; “afadhali nikae kimya” huku idadi kubwa ya mashabiki wakionyesha kukerwa na ujumbe huo uliosambazwa mara 16,000 kwenye mtandao wa Internet.
Janga la Ebola limesababisha vifo vya zaidi ya watu 4,000 katika kanda ya Afrika Magharibi na kuenea hadi nchini Hispania na Marekani.

0 Comments: