Friday, October 17, 2014

Tonto Dikeh amuunga mkono Genevieve Nnaji

LAGOS, Nigeria
MWAKA 2012, mwigizaji wa Nollywood, Tonto Dikeh alisema shoga yake Genevieve Nnaji wana ushirikiano mzuri katika sekta ya filamu za Afrika na mwigizaji huyo amedhihirisha hilo kwa kutoa msaada wake kwa mwanadada huyo. 

Nnaji hivi karibuni alianzisha mavazi yake, ambapo amekuwa akipokea ujumbe wa pongezi kutoka kwa shoga yake, Dikeh na marafiki mbalimbali. 

Dikeh amekuwa mmoja wa watu walioonyesha msaada na kumpigia kelele kwenye vyombo vya habari vya kijamii mwanadada Diva.
“Pongezi Genevieve juu ya mradi wako mpya, neema na nguvu, upendo uwe juu yako malkia G,” alisema Dikeh.


0 Comments: