Leo usiku, ndani ya Jiji la Johannesburg, kitongoji
cha Soweto, katika viwanja vya Watler Sisulu, zinafanyika kwa mara ya tisa,
tuzo za video bora za muziki Afrika zinazoratibiwa na kituo cha Televisheni cha
Channel O, huku Tanzania ikiwa na wawakilishi wawili wanaowania jumla ya tuzo
nne.
Hii siyo mara ya kwanza kwa wanamuziki hawa kutajwa
kuingia katika tunzo hizi zinazodaiwa kuwa za pili kwa ukubwa Afrika ukiachana
na ile ya Kora, kumbukumbu za gazeti hili zinaonyesha mwaka jana pia wanamuziki
hawa wakiwa na mwenzao wa kike Sarah Kais walikwenda huko huko Afrika ya
Kusini, na kurudi wakiwa hawajaambulia hata tunzo, na katika uchunguzi wetu
tukagundua kwamba kwetu hapa huwa si watendaji sana kwenye suala la kura.