Tamasha la Ngoma za asili la makabila ya mkoa wa Mtwara Maarufu
kama Tamasha la MaKuYa limeanza rasmi, huku vikundi mbalimbali vya sanaa
vikonyesha umahiri mkubwa katika kucheza ngoma za asili za makabila
yao.
Tamasha
hilo ambalo mwaka huu lilianza kwa maandamano kutoka katika viwanja vya
mashujaa kwenda Uwanja wa Nangwanda maarufu kama uwanja wa Umoja mjini
Mtwara limevuta hisia za wakazi wengi wa mji wa huo na vitongoji vyake
ambapo licha kuwepo kwa jua kali lakini watu waliendelea kumiminika
uwanjani kushuhudia wasanii wakisakata ngoma mbalimbali.
0 Comments:
Post a Comment