Leo usiku, ndani ya Jiji la Johannesburg, kitongoji
cha Soweto, katika viwanja vya Watler Sisulu, zinafanyika kwa mara ya tisa,
tuzo za video bora za muziki Afrika zinazoratibiwa na kituo cha Televisheni cha
Channel O, huku Tanzania ikiwa na wawakilishi wawili wanaowania jumla ya tuzo
nne.
Hii siyo mara ya kwanza kwa wanamuziki hawa kutajwa
kuingia katika tunzo hizi zinazodaiwa kuwa za pili kwa ukubwa Afrika ukiachana
na ile ya Kora, kumbukumbu za gazeti hili zinaonyesha mwaka jana pia wanamuziki
hawa wakiwa na mwenzao wa kike Sarah Kais walikwenda huko huko Afrika ya
Kusini, na kurudi wakiwa hawajaambulia hata tunzo, na katika uchunguzi wetu
tukagundua kwamba kwetu hapa huwa si watendaji sana kwenye suala la kura.
Mwaka huu zimekuwapo kampeni kila kona ya nchi, za
kila aina, na mpaka tamasha la kuomba kura likafanyika ili mwisho wa Tanzania
nayo iingie kwenye ramani ya kimataifa ya muziki kwa kuwa na mwanamuziki
aliyetukuka kutokana na sanaa yake hiyo.
AY anawania jumla ya tunzo tatu
Ya kwanza ni Most Gifted East African Video, ambapo
wimbo wa I dont wanna be Alone, AY na Sauti Sol umeingia, yeye hapa anapambana
na Keko akimshirikisha Madtraxx katika Make You Dance,
Camp Mulla nao wanawania tunzo hii hii kupitia wimbo
Party Donít Stop, KíNaan akimshirikisha Nas katika Nothing To lose na mwisho
kabisa anayewania tunzo hii ni Navio kwa kutumia wimbo wake One & Only Ya
pili ni Most Gifted Video of the Year, wimbo wake Speak with your Body, AY
ameshirikiana na Romeo na Lamaya. tunzo hii inawaniwa na watu 10!
Hapa wengine wanaowania tunzo hii hii ni:
DJ Zinhle Feat. Busiswa - My Name Is
Khuli Chana Feat. Notshi - Tswa daar
Toya Delazy - Pump It On
Lizha James Feat. Perola - Leva Boy
Big Nelo - Sente beat
Díbanj - Oliver Twist
Brymo - Ara
Sarkodie Feat. Obrafour - Saa Okodie No
Camp Mulla - Fresh all day
Na wimbo huo huo Speak with your Body unaingia kwenye
kundi la Most Gifted male Video na hapa anapambana na Oliver Twist ya D Banj
kutoka Nigeria, na Big Nelo wa Angola ambaye ameingia, Pro kutoka Afrika ya
kusini na wimbo wake Makasana na wimbo wake Sente O’ Beat.
CPwaa
Yeye anawania tunzo moja ya Most Gifted Dance Video of
the year” kupitia wimbo wake wa Hnmmm abapambana na DJ Zinhle akimshirikisha
Busiswa katika My Name Is, DJ Cleo pia anawania tunzo hii hii na wimbo wake
Facebook, OS3 kwa kushirikiana na Tchoboly kupitia wimbo Mokongo pia wamo
katika kuwania tunzo hii pamoja na Davido kupitia wimbo Dami Duro pamoja na
Bucie kupitia Get Over It!
Picha inaonekana wazi kwamba wanamuziki wetu wako
katika wakati mgumu ukilinganisha na watu wanaoshindana nao katika tunzo hizi
ingawa kila mtanzania ana matumaini kwamba safari hii inawezekana wasanii wetu
wakarudi na tunzo ambazo zitasababisha sanaa ya kitanzania kuwa katika ramani
nzuri kama ulivyo utalii wetu pia.
Tofauti na nchi za wenzetu, tanzania kwa upande wa
sanaa, hasa ya muziki, Jiji la dar es salaam pekee linaonekana kuwa na muamko
wa kusaidia wasanii katika kampeni za kimataifa za kimuziki kuliko mikoa
mingine ambapo wamekuwa ni mashabiki wa kusubiri burudani tu.
AY kwa upande wake alisema,” mi nashukuru kwa watu
wote walionisupport maana kusupport AY ni kusupport muziki wa Tanzania,
magazeti, TV na Radio stations na blogs, mitandao ya kijamii na wote
walioonyesha nia.
Nawashukuru sana,yale ni mashindano na kila mtu
anavyoenda kule anaenda akiwa na moyo wa kushindana, ila ukiwa mshindani
ukubali kuna kushinda na kushindwa kutokana na kura zilizopigwa so natumai watu
walipiga vya kutosha. categories zote ziko tough but I believe tutafanikisha
zote au moja”.
Mungu ibariki Tanzania, Mungu
wabarariki wasanii hawa walete heshima kwa nchi yao
Source: Henry Mdimu
All the Best TeamTanzania in South Africa for CHANNEL O MUSIC VIDEO AWARDS #CHOMVA2012







0 Comments:
Post a Comment