Thursday, July 19, 2012

YVONNE CHAKA CHAKA KUFUNGUA SHULE YA MUZIKI KWA WATOTO NAIROBI

Mwanamuziki mkongwe wa nchini Afrika Kusini na ambaye inasemekana alikuwa ni mtoto wa kwanza mweusi kuonekana kwenye Television za nchini Afrika kusini enzi za utawala wa Mkaburu, Yvonne ChakaChaka atatimba nchini kenya mwishoni mwa mwezi wa nane katika ufunguzi wa shule maalumu ya watoto ya muziki, ijulikanayo kama Maisha Mapya Music Centre mbao unategemea kufanyika katika viwanja vya Carnivore jijini Nairobi.

Yvyone amealikwa na kundi la wajasiriamali ambaeokwa pamoja wamejiunga na kuanzisha shule hii ambayo itakuwa maalumu kwa watoto wenye umri wa miaka 6 na miaka 12. Wilfred Opiyo mmoja wa wajasiriamali na waanzilishi wa shule hii, aliviambia vyombo vya habari kwamba shule hii maalumu itakuwa Nairobi Primary School, na kwamba itakuwa ikitoa mafunzo ya kutumia vifaa mbali mbali vya muziki zaidi ya 50. Watoto watapata chance ya kuamua kifaa gani wangependa kutumia katika muziki, na kukisomea zaidi kifaa hicho, mbali na hayo center hiyo itatoa huduma mbali mbali za muziki nje na ndani ya darasa.

0 Comments: