Thursday, July 19, 2012

Genevieve Nnaji balozi wa Range Rovers( Nigeria)


Kwa wale wapenzi wa Filamu za Kinaija( Nigeria) lazina Genevieve Nnaji utakuwa unamnyaka ama unamwona au kumsikia sikia. Kama humnyaki basi hii ndio nakupa nyeti nyingine. Genevive mzaliwa wa Mbaise, Imo State ndani ya Nigeria ni miongoni mwa wadadada ambao wamepata mafanikio katika uchezaji wa filamu nchini Nigeria.

Hivi karibuni mwanadada huyu amejipatia chance kubwa kwa kuchaguliwa kuwa balozi wa mikoko mikali mipya aina ya Range Rover Evoque. Dili hili ambalo litampatia mwanadada huyu mkwanya wa mamilioni ya Naira za ki "naija" litamfanya aishi maisha ya raha mustarehe kwani atakuwa akiruka mara kwa mara nje na kukutana na mabalozi wengine wa magari ya aina ya Land Rover kama Victoria Backham na wengine kibao. Ginevieve baada ya kuchaguliwa alikabidhiwa mkoko mpya wa aina ya Range Rover Evoque ambao ndio atakuwa akiuza nao sura katika sehemu mbalimbali.

0 Comments: