Friday, July 20, 2012

SHILOLE AKANUSHA UVUMI WA UHUSIANO WAKE YEYE NA BARNABA

Zilizoajiri kitaani ambazo hata mimi nilizinyaka na kuchuna kiaina, kulikuwa na uvumi kwamba Mwanadada Shilole.... weeeeeee..... kwamba alikuwa na uhusiano wa chini chini na msanii mwenye manjonjo saaana katika sauti yake, kufikia hadi kukubaliwa na mkongoliz FALLY IPUPA, hapa namzunguzia, mzee wa "magube gube".. ah sorry yani jamaa aliyeimba wimbo wa magube gube Barnaba... ehh kufikia hadi kuwa kama dereva wake kwamba alionekana onekana kitaa akiwa anaendesha gari la shilole. duh.. watu bwana..

Katika YOU HEARD, na Sudy Brown, kupitia kipindi cha XXL ya Clouds FM, Shilole ametupilia mbali Uvumi huo na kusema kwamba yeye na Barnaba ni washkaji tu, na kuhusiana na kumfanya Dereva, hilo halipo kabisa..
Hehehee....

Sudy Brown alivuta waya na kumpigia mke wa Barnaba, mama steve, naye alisema hajasikia uvumi huo, lakini yeye anampenda Barnaba, na kwamba akicheza nje acheze tu wakimwacha anajua atarudi kwake.. WHAT, the,......... WHAT!!!!!

Barnaba

0 Comments: