Friday, July 20, 2012

JUA KALI AOKOA MAISHA YA WATU KATIKA NDEGE

Msanii mkali nchini Kenya, JUA CALI ameokoa maisha ya watu kibao waliokuwa wakiwa katika ndege ambayo muda mchache ilitakiwa kuruka kutoka uwanja wa ndege nchini Amsterdam. Story hizi nimezinyaka katika mtandao mmoja wa Habari kuanika kwamba, Akiwa katika safari zake za kimziki barani Ulaya, Jua Cali alistukia inshu hii akiwa katika uwanja wa ndege Amsterdam, baada ya kupanda katika ndege, na kuketi katika seat yake ambayo ni ya upande wa dirisha.

Jua Cali katika kucheki cheki dirishani akaona moshi mdogo mdogo ukitoka katika injini ya ndege, baada ya hapo akamuita muhudumu wa ndege hiyo na kumpa taarifa, Mhudumu huyo alipoona hivyo akatoka mkuku na kwenda kumwambia Pilot na baada ya hapo watu wote waliambiwa kushuka kwenye ndege. Duh, inasemekana kwamba hamna aliyeona tatizo hilo zaidi ya Jua Cali.

Baada ya hapo Airport ilimlipia Jua Cali safari yake, na pia kupewa 10 bonus Fisrt Class Tickets ambazo zinatakiwa zitumike kabla ya miaka 5 kuisha.
Zawadi Gani Hii?, mi naona He Deserve more than This.. ahhh

0 Comments: