Thursday, July 19, 2012

REDSUN NA DEAL KUBWA

Mkali wa Miondoko ya Dance Hall nchini kenya, Redsun amekula dili kubwa na kusign mkataba na kampuni ya UrFilez, kampuni kubwa ya usambazaji wa muziki kupitia mitandaoni 24/7 kupitia kampuni ya Rapid Communications. Redsun ni mmoja wa wasanii wachache wa Africa waliopata nafasi hii ambapo wapenzi wa muziki wake watapata nafasi ya kusikiliza na kununua kazi za msanii huyu kwa muda wote na popote duniani.

Mbali na kupata chance ya kusikiliza kazi za wasanii, pia watapata nafasi ya kupata habari zozote kuhusiana na msanii Redsun, na wengine waliosign mkataba na kampuni ya Rapid Communications. Hivi karibuni wakati wa kusign mkataba huo, Mmiliki wa mtandano huu, Mr Anwar Hussein, amesema mtandao wa Ur Filez utaanza kazi katika nchi za Kenya, Ethiopia, Uganda, Tanzania, Sudan na pia Jamhuri ya Democrasia ya Congo. Ur Filez wanampango wa kuwa mstari wa mbele katika maswala ya Digital Music Technology na kuhakikisha watumiaji wa mitandao wanapata huduma iliyo ya kiwango katika muziki, kitaifa na kimataifa.

0 Comments: